Bunge lapitisha BAJETI kwa mwaka wa fedha 2019/2020

0
401

Serikali imewahakikishia wakulima wa mazao ya Pamba na Korosho nchini, upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao hayo kwa kushirkiana na mataifa mbalimbali duniani wenye uwezo wa mazo  kwa bei yenye manufaa kwa wakulia wa mazao hayo.

Wakijibu hoja za wabunge juu ya hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashingwa na Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba wamesema tayari Seikali imeshakutana na wadau mbalimbali wa mazao hayo ambao wameonyesha nia ya kunua mazao hayo.

Pamoja na mambo mengine, lakini suala kuhusu upatikanaji wa masoko ya uhakika juu ya mazao ya Pamba na Korosho, mawaziri wenye dhamana walitoa kauli ya serikali.

Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji akaeleza nia ya serikali katika ujenzi wa viwanda vya Taulo zakike, huku waziri Dokta Phillipo Mpango akiliomba bunge kupitisha bajeti hiyo ili kuleta manufaa kwa wananchi.

Mara baada ya mjadala huo Bunge limetpisha bajeti ya serikali kiasi cha Shilingi Trilioni 33.1 kwa mwaka wa fedha 2019/2020.