Bunge lapitisha Bajeti Kuu ya Serikali 2022/23

0
155

Bunge limepitisha bajeti Kuu ya serikali ya shilingi trilioni 41.48 kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Akisoma idadi ya kura za wabunge waliopitisha bajeti hiyo Spika wa bunge Dkt. Tulia Ackson amesema idadi ya wabunge waliopiga kura ni 379, waliosema ndio ni 356, hakuna waliosema hapana na ambao hawakuamua ni 23 hivyo idadi ya wabunge waliosema ndio wamepitisha bajeti hiyo kwa asilimia 94.