Bunge la Tanzania na China kushirikiana katika kukuza Demokrasia

0
238

Bunge la Tanzania na China kushirikiana katika kukuza Demokrasia

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemuahidi Naibu spika wa Bunge la China Ji Bing Xuan kuwa bunge lake litaendelea kushirikiana na Bunge la China katika kukuza Demokrasia katika nchi hizo mbili.

Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe wa Naibu spika wa Bunge la China, Spika Ndugai amesema kuwa kwa sasa nchi hizo mbili zimekuwa na mashirikiano ya karibu hivyo wataendeleza ushirikiano huo kwa lengo la kukuza Demokrasia.

Ndugai amemueleza Spika Xuan kuwa wanaangalia uwezekano wa kila bunge kuweka utaratibu wa wabunge wa nchi zote mbili kutembeleana

Kwa upande wake Naibu Spika Xuan amemueleza Spika Ndugai na Ujumbe wake kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kupiga hatua za kimaendeleo na hasa ujenzi wa viwanda