Boti yazama, watu 150 hawajulikani walipo

0
279

Takribani watu 150  hawajulikani walipo baada ya boti waliyokua wakisafiria kuzama katika ziwa Kivu,  lililopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, tayari miili ya watu watatu waliokufa maji imepatikana na watu wengine 33 wameokolewa wakiwa hai.

Rais Tshisekedi amesema kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za ajali ya kuzama kwa boti hiyo na atahakikisha chanzo cha ajali hiyo kinafahamika na endapo ni uzembe,  wote waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria.