BOT yasema noti zake hazihusiki na usambazaji wa corona

0
285

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo zimekua zikisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, zinazohusisha noti za BOT na usambazaji wa virusi vya corona.
 
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya benki hiyo imesema kuwa noti za BOT zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti hizo.

Hata hivyo kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, BOT imewashauri Watanzania kuzingatia miongozi mbalimbali inayotolewa na mamlaka zenye dhamana ya afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni ama vitakasa mikono (sanitizers)  ili kuua vimelea kwenye mikono.