Bosi trafiki apiga marufuku magari ya mizigo kubeba abiria

0
277

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa amewaagiza wakuu wa vikosi hivyo katika mikoa yote nchini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye magari ya mizigo yanayopakia abiria, kisha kuwashusha abiria hao na kuchukua hatua kali kwa madereva.

Kamanda Mutafungwa ametoa agizo hilo baada ya kukagua eneo ilipotokea ajali ya gari la kubeba magazeti, na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine watatu kujeruhiwa katika kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Aidha Mkuu huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini amepiga marufuku magari yanayosafirishwa nje ya nchi maarufu IT kupakiza abiria kwa kuwa hayaruhusiwi kufanya hivyo.