Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo imeeleza kuwa, Profesa Mbarawa ameivunja Bodi hiyo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu namba 14 cha jedwali la kwanza la Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira namba Tano ya Mwaka 2019, kikisomwa pamoja na kanuni Namba 14 ya kanuni za usambazaji wa maji.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bodi ya MORUWASA imevunjwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia mamlaka ya maji, na hivyo kuathiri utoaji wa huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Morogoro.
Kufuatia uamuzi huo, Waziri Mbarawa ametaka kuanza kwa utaratibu utakaowezesha kuundwa kwa Bodi mpya.