Bodi ya TRC yavunjwa

0
232

Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Mhandisi John Nzulule.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Rais amesema Watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.