Bodi ya Mikopo yaweka mazingira mazuri kwa wadaiwa sugu.

0
938


Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wadaiwa wa bodi hiyo ambayo hadi sasa inadai shilingi Bilioni 291 kwa wadaiwa sugu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Abdul Razaq Badru amesema katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2018 Bodi ya mikopo imekusanya jumla ya shilingi bilioni 94 na kuvuka lengo la kukusanya bilioni 71 katika kipindi hicho.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari bodi ya mikopo imetangaza rasmi kujiunga na mfumo wa serikali wa ukusanyaji mapato yaani (Government e-payment Gateway – GEPG) na kusisitiza kuwa malipo yote kwenda bodi ya mikopo yatapokelewa kwa mfumo unaofuatwa na taasisi za serikali.