Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Innocent Bashungwa amesema hadi kufikia Januari, 2022 shilingi bilioni 9.3 kwa ajili ya kuendeleza sera ya elimu bila ada Mkoani Kagera.
Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Utumishi wa Kiaskofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Lulenge – Ngara Mkoani Kagera.
Waziri Bashungwa amesema Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa ya shule za sekondari na msingi 167 na kuwezesha kujenga maabara 72 lengo ni kupunguza uhaba wa maabara mashuleni.
Sambamba na hilo Waziri Bashungwa amesema mkoa wa Kagera kulikuwa na kata 11 ambazo hazikuwa na shule za Sekondari hivyo, Serikali imetoa shilingi bilioni 7.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari kwenye kata ambazo hazikuwa na shule za Sekondari.
Waziri Bashungwa ameendelea kusema kwa Mkoa wa Kagera kiasi cha shilingi bilioni 15 . zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 116 ya shule za sekondari ambayo yamewezesha kupunguza msongamano mashuleni.