Bilioni 5 kujenga hospitali ya kanda Kigoma

0
242

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Kanda mkoani Kigoma.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo mkoani Kigoma wakati akizungumza na wakazi wa manispaa ya Kigoma – Ujiji mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi na upanuzi wa hospital ya rufaa Maweni na kusisitiza kuwa anataka mkoa huo uimarike kila sekta.

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe hilo la msingi katika ujenzi na upanuzi wa hospital ya rufaa Maweni, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma.