Bilioni 450 kukamilisha mradi wa bandari Tanga

0
181

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Eric Hamis amesema mara baada ya kukamilika kwa mradi uongezaji kina Bandari ya Tanga kutasaidia kurahisisha upakuaji wa shehena bandarini hapo, na kupunguza gharama zilizokuepo awali.

Amesema hayo wakati akitoa maelezo ya mradi huo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Mradi huo unatarajia kukamilika Novemba 2022 na zaidi ya shilingi bilioni 450 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo.