Bilioni 362 kutumika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

0
202

 
Serikali imeanza kutumia shilingi bilioni 362 zilizotengwa kwenye mwaka wa fedha wa 2021/2022, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Selemani Jafo alipokuwa akitoa msimamo wa Tanzania wakati wa  majadiliano ya mkutano wa 26 wa nchi Wananchama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Amesema miradi hiyo inatekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Nishati, Misitu, Viwanda na TEHAMA pamoja na kujenga uwezo wa kitaasisi.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo, athari za mabadiliko ya Tabianchi zimeilazimu Serikali kutumia asilimia mbili mpaka tatu ya pato la Taifa katika kukabiliana nazo.