Bilioni 30 kujenga Makao Makuu ya Uhamiaji

0
187

Serikali imepanga kutumia Shilingi Bilioni Thelathini katika mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dodoma.

Mpango huo wa serikali umetangazwa jijiji Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhani Kailima alipofanya ziara katika eneo la ujenzi wa mradi huo.