Bilioni 3.7 kutumika kujenga na kukarabati Mialo na Masoko

0
170

Serikali unatarajia kutumia kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 3.7, kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa mialo na masoko kwa kuweka miundombinu mbalimbali ya kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na kupunguza upotevu baada ya kuvunwa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, wakati wa mkutano wa pamoja baina ya uongozi wa soko la samaki la Ferry Dar es Salaam, wavuvi pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo kwa ajili ya kuzungumzia maboresho ya soko hilo yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza katika mkutano huo ulioudhuriwa pia na Naibu wizara hiyo Abdallah Ulega, Ndaki amesema pamoja na idadi ya wavuvi wanaokadiriwa kufikia Milioni 4.5 waliopo, Serikali imekuwa haipati pato la kutosha kutoka katika sekta hiyo hatua inayosababishwa na kutokuwepo kwa miundombinu rafiki ya uvuvi na uhifadhi wa samaki.

“Lengo ni kuhakikisha tunawawezesha wavuvi kuongeza ufanisi na tija katika kazi yao, sambamba na kuongeza mchango wao katika pato la Taifa, mwaka 2021 pato la Taifa ilikuwa ni asilimia 1.7, tunakusudia siku zijazo pato hili likue,” amesema Ndaki.

Ukarabati wa soko hilo linalohudumia wafanyabiashara 10000 kwa sasa kutoka malengo la idadi ya idadi ya wafanyabiashara 1500 waliokuwa wamekadiriwa mahali hapo, utalifanya liweze kuhimili ongezeko hilo na kutoa huduma zake kwa ufanisi.