Wizara ya Viwanda Uwekezaji na Biashara imesema Tanzania ipo tayari kuzalisha kwa wingi ili bidhaa zake ziweze kuingia katika soko la eneo huru la biashara barani Afrika.
Hayo yamesema na Waziri wa wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akizungumza katika Hafla ya ufunguzi wa maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendela katika viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.
Dkt. Kijaji amesema kuwa katika maonesho hayo wapo wafanya biashara mabalimbali kutoka nje ya nchi ambao wanatumia teknolojia na mashine za kisasa kuzalisha hivyo wizara itashirikiana nao kupata mbinu na ujuzi wa teknolojia hizo ili kuendela kuzalisha bidhaa bora kwa wingi na kuifikia dunia.