Benki ya NMB yaiongezea nguvu sekta ya kilimo

0
109

Benki ya NMB imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 220 kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo kupitia mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 9

Akizungumza katika maonesho ya kimataifa ya biashara mkuu wa kitengo cha kilimo biashara kutoka benki hiyo Isack Masusu amesema benki hiyo ipo tayari kutoa mikopo ya vifaa na pembejeo za kisasa ili kuwezesha watanzania kuzalisha bidhaa zenye viwango zitakazoweza kushindana katika soko huru la Biashara barani Afrika.