Bei ya mbolea ya urea yashuka bei

0
273

Serikali imetanga bei elekezi ya kuuza mbolea aina ya urea, itakayoanza kutumika Februari 20 mwaka huu.

Bei hiyo elekezi imetangazwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ambapo mfuko wa kilo 50 utauzwa kwa shilingi 51,500 kutoka shilingi 54,000 za awali.

Bei hiyo ni nafuu kwa shilingi 2,500 ikilinganishwa na bei iliyokua ikitumika siku za nyuma.