Upatikanaji wa dagaa wa ziwa Tanganyika maarufu kama wa dagaa wa Kigoma umeongezeka, na kusababisha bei ya bidhaa hiyo kushuka kutoka Shilingi Elfu Thelathini kwa kilo Moja hadi kufikia Shilingi Elfu Kumi na Tatu.
Mwandishi wa TBC mkoani Kigoma, -Egidius Audax ametembelea soko la Kibirizi lililopo katika Manispaa ya Kigoma ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa dagaa hao.