Basi la Bright Line lapata ajali Shinyanga

0
186

Basi la Bright Line lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Dodoma limepata ajali katika eneo la Isela barabara ya Shinyanga – Tinde baada ya kugongana na gari dogo na pikipiki leo Jumatatu Januari 13,2020 majira ya saa nne asubuhi.

Taarifa za awali zinasema kuna vifo na majeruhi kadhaa.

Inaelezwa kuwa mwendesha bodaboda na abiria wake wamepoteza maisha na bado wamelaliwa na basi hilo.