Bashungwa aipongeza Yanga kwa ubingwa 2021/22

0
255

Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa ameipongeza Yanga SC kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya mpira wa miguu msimu wa 2021/22 unaowapa fursa ya kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika.

Ametoa pongezi hizo Juni 25, 2022 jijini Mbeya wakati akikabidhi kombe kwa bingwa wa ligi kuu msimu huu baada ya mchezo kati ya Mbeya City na Yanga katika Uwanja wa Sokoine.

Bashungwa baada ya kukabidhi kombe hilo, amempongeza Rais Samia Suluhu hassan kwa juhudi kubwa za kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini kwa kasi ya kubwa na amekuwa akitoa miongozo, maelekezo, motisha na uwezeshaji mkubwa katika mchezo wa mpira wa miguu na sekta nzima.

Ametoa wito kwa wanamichezo kuendelea kujituma kwa kuwa michezo ni ajira, kwa sababu wachezaji huibuliwa na kuanzia ngazi za chini.

Aidha, amevitaka vyama na vilabu vya michezo kushiriki katika michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ili kupata vipaji vya kuendeleza sekta hii na kwa mashindano hayo ngazi ya wilaya na mikoa.