BASHE: Riba ya 18% … labda ulime bangi

0
275

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameomba benki kupunguza riba inayotozwa kwenye kilimo ya asilimia 18% na 20% kwani riba hiyo ni kubwa.

Akizungumza na washiriki wa maonesho ya kilimo, uvuvi na ufugaji (Nanenane) yanayofanyika Nyakabindi, Simiyu katika shughuli iliyoandaliwa na Kanda ya Ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga) kwa ajili ya kuhamasisha vijana kushiriki katika kilimo, Bashe amesema, “Riba ya 18% na 20% kwenye kilimo haiwezekani, labda ulime bangi. Tunaomba iweze kufika hata 10%.”

Aidha, Bashe ameonesha kupendezwa na mwitikio wa wanawake katika maonesho hayo.

Akizungumza na washiriki wa maonesho hayo Bashe amesema, “nawapongeza wakina mama kwa mwitikio wao katika maisha haya.”

Katika kusisitiza, ameongeza kuwa asilimia 70% ya walioshiriki katika maonesho haya ni wakina mama.