Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na michoro ya barabara ya Kongwa, Mpwapwa hadi Kibakwe mkoani Dodoma ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuondoa changamoto ya ubovu wa barabara iliyopo hivi sasa.
Waziri Mkuu Majaliwa amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia ombi la Wabunge wa wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake wilayani humo na kuongeza kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo zitatengwa katika mwaka ujao wa fedha wa 2018/2019.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Dodoma ambayo aliikatisha kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
Akiwa wilayani Mpwapwa, Waziri Mkuu Majaliwa pia amewaagiza watendaji wa vijiji na kata wilayani humo kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaojihusisha na uharibifu wa vyanzo vya maji na kusababisha wilaya hiyo kuwa na vyanzo vichache vya maji.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na michoro ya barabara ya Kongwa, Mpwapwa hadi Kibakwe mkoani Dodoma ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuondoa changamoto ya ubovu wa barabara iliyopo hivi sasa.
Waziri Mkuu Majaliwa amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia ombi la Wabunge wa wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake wilayani humo na kuongeza kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo zitatengwa katika mwaka ujao wa fedha wa 2018/2019.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Dodoma ambayo
aliikatisha kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.