Barabara nchini Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati Mtanzania

0
565

Ujerumani inakusudia kuipa moja ya babrabara zake jina la mwanaharakati wa kisiasa kutoka Tanzania, ambapo kwa sasa barabara hiyo ina jina la aliyekuwa Gavana wa Afrika Mashariki wakati wa ukoloni aliyeamuru watu kuuawa.

Barabara ya Wissmannstraße ambao unaotokana na jina la Gavana Hermann von Wissmann utabadilishwa na Mtaa wa Lucy Lameck (Lucy-Lameck-Straße). ‘Straße’ ni neno la kijerumani likiwa na maana ya barabara.

Lucy Lameck alikuwa ni mwanamke wa kwanza Mtanzania kuwa kwenye baraza la mawaziri na pia mtu muhimu katika kupigania uhuru.

“Tumemchagua mwanaharakati wa Tanzania tofauti na Von Wissman, kwa sababu yeye alipambana kukomesha ukoloni na ubaguzi wa rangi,” kimesema chama cha Berlin Postkolonial, ambacho ni moja ya vyama vilivyoshiriki kuleta mabadiliko nchini Ujerumani.

Lameck alizaliwa mkoani Kilimanjaro mwaka 1934 katika familia ya wakulima na alikuwa muugizi kabla ya kugeukia siasa.

Anatambuliwa kama mwanamke aliyetumia karibu maisha yake yote katika kuboresha maisha ya wanawake nchini Tanzania.