Balozi Wa Ufaransa Nchini Apongezwa Kwa Kuzungumza Kiswahili

0
173

Rais John Magufuli amempongeza Balozi wa Ufaransa hapa nchini Federic Clavier kwa kuzungumza ka ufasaha Lugha ya Kiswahili licha ya kwamba yeye ni Mfaransa.

https://www.youtube.com/watch?v=kcIBEypeJyY&t=4s

Pongezi hizo za Rais Magufuli amezitoa jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Rada Mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

“Huyu ni Mfaransa, lakini tumesikia wote jinsi alivyoongea kiswahili hapa, sasa unakuta mtu ni wa hapahapa bongo anafikiri kuongea Kiingereza ndio kujua, naomba niwaambie ni kupungukiwa”, amesema Rais Magufuli.

Ameendelea kuwasisitiza
Watanzania kuithamini na kuienzi lugha ya kiswahili, kwani lugha hiyo imeanza kukua na kuenea katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki na Kati.