BAKWATA: Somo la dini lirasimishwe

0
152

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limeiomba Serikali kurasimisha somo la dini katika shule mbalimbali nchini, ili kulinda maadili kwa watoto na vijana wa Kitanzania katika umri mdogo.

Akisoma tamko la BAKWATA katika Baraza la Eid El Fitri, Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikh Nuhu Mruma amesema, kurasimishwa kwa somo la dini kutalinda maadili ya vijana tangu wakiwa shule na kuondoa mmonyoko wa maadili unaooneka katika jamii kwa sasa.

BAKWATA pia imeiomba Serikali kuajiri walimu wa masomo ya dini na wawe sehemu ya walimu katika shule na vyuo vya Serikali.

Sheikh Mruma ametoa wito kwa Wananchi kulinda maadili ya Kitanzania na kukemea vitendo viovu vinavyoonekana kushamiri kwa sasa.