Bajeti ya TAMISEMI yapita

0
163

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 yenye jumla ya shilingi Trilioni 9.1.

Kati ya fedha zinazoombwa, shilingi Trilioni 5.6 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara ambayo ni shilingi
Trilioni 4.5, matumizi mengine shilingi Trilioni 1.06 na shilingi Trilioni 3.4 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.