Baba mbaroni kwa kumwozesha binti wa miaka 11

0
132

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Emuguru wilayani Same kwa tuhuma za kumuozesha binti yake mwenye umri wa miaka 11.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Simon Maigwa amesema tayari baba huyo alishapokea mahari ya ng’ombe watatu kutoka kwa muoaji.

Kamanda Maigwa amesema kabla ya mtuhumiwa kukamatwa alishafanya sherehe ya kimila tarehe Agosti 7, s2021 nyumbani kwake kumuaga binti huyo kwenda kwa mume wake.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limetoa onyo kali kwa watu wenye tabia za kuozesha watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18 kwani ni kinyume cha sheria.

Sauda Shimbo- Same