Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umefikia makubaliano na kampuni ya Azam Marine ya kutoa huduma ya kuvusha abiria kati ya Magogoni na Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
TEMESA imesema lengo ni kuendelea kuwapa wananchi huduma za uhakika wakati huu ukiendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake.
Aidha, umeshauri wananchi kuacha kutumia mitumbwi kuvuka, ili kulinda usalama wao.