Aweso aahidi kupeleka maji shule ya Benjamin

0
245

Waziri wa maji Jumaa Aweso ameahidi kupeleka maji Katika shule Sekondari Benjamin Mkapa ya iliyopo jijini Dar es Salaam mara baada ya ombi la Mkuu wa shule hiyo kueleza uhitaji wa maji shuleni hapo wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyokuwa ameahidi kuwatembelea

“Nimemsikia Mkuu wa shule hapa akisema wanatumia visima viwili vya maji, lakini wanahitaji pia maji ya DAWASA, sasa Niwaagize DAWASA kuleta maji hayo hapa shuleni Ili wayatumie kwa shughuli zao” ameongeza waziri Aweso

Rais Samia amefanya Ziara hiyo baada ya kuaidi kufika shuleni hapo mara baada ya kuongea kwa simu na Mwanafunzi wa shule hiyo Emmanuel Mzena wakati TBC ikirusha Mbashara siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 27 Januari mwaka huu