Auawa ndani ya nyumba yake

0
581

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Colletha Francis,  Mkazi wa kijiji cha Ihunga wilayani Muleba mkoani Kagera  ameuawa kwa kuchomwa moto akiwa ndani ya nyumba yake  na watu wasiojulikana.

Chanzo cha mauaji hayo kinaelezwa ni kupotea kwa mtoto  Ismail Khamis toka Aprili Tano mwaka huu na mwili wake kukutwa umezikwa shambani kwa mwanamke huyo.

Imeelezwa kuwa mwili wa mtoto huyo uligundulika umezikwa katika shamba la Marehemu Colletha ukiwa wima, baada ya mbwa aliyekuwa akipita maeneo hayo kufukua sehemu hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Muleba, -Richard Ruyango amefika katika kijiji hicho cha Ihunga na kuwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi huku akiwataka viongozi wa dini kuingilia kati suala hilo kwa kuzikutanisha familia mbili zilizokumbwa na vifo hivyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera, – Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa kifo  cha Colletha na kupatikana kwa mwili wa mtoto huyo.