Atiwa nguvuni na Polisi kwa kumpa ujauzito mwanafunzi

0
189

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Samweli Lifa (24), mkazi wa wilaya ya Kilosa kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kwanza (mwenye miaka 16) anayesoma Shule ya Sekondari Mikumi Day iliyopo wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu amesema mtuhuniwa huyo alimndanganya mwanafunzi kuwa atamuona baada ya kumaliza masomo, lakini mara baada ya kutimiza lengo lake la kumbaka na kumpa ujauzito alikimbia kusikojulikana na baadaye jeshi hilo likamtia nguvuni.

Kamanda Muslimu ametoa wito kwa jamiii kuacha tabia ya kuwadanganya wanafunzi kwani jeshi hilo halitawaacha salama.