ATCL yaongeza safari

0
137

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake za ndani na nje ya nchi, kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
 
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa  ATCL  Josephat Kagirwa amesema  safari zilizoongezwa ni pamoja na za Dodoma- Mwanza, Dar es Salaam – Mtwara,  Dar es Salaam – Bujumbura,  Dar es Salaam – Lubumbashi pamoja na Dar es Salaam  – Nairobi.
 
Kagirwa amesema ongezeko la safari hizo ni linatokana na ujio wa ndege mbili hivi karibuni na ni  utekelezaji wa mpango mkakati wa shirika hilo,  ambapo lilijipanga  kupanua safari zake kwa kuongeza ndege.
 
Akizungumzia ujio wa ndege hizo  aina ya Airbus A220-300, Kagirwa  amesema zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 132, na kati ya hao 12 wa daraja la biashara na 120 daraja la uchumi.