Rais John Magufuli amesema kuwa, hamu kubwa la Watanzania kwa sasa ni kuona nchi yao inapiga hatua za Kimaendeleo huku akisisitiza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linamiliki asilimia 75 ya soko la usafiri wa anga hapa nchini ukilinganisha na asilimia Tatu za miaka mitatu iliyopita.
Rais Magufuli amesema kuwa, kwa sasa ATCL imeanza kutanua huduma zake na kuingia katika soko la Kimataifa na tayari imeanza kufanya safari zake katika nchi za Comoro, Burundi, Uganda, Zimbabwe, Zambia na India.
Akihutubia wakati wa uzinduzi wa Rada Mbili za kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijjini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema kuwa, hivi karibuni ATCL itaanza kwenda nchini China na maeneo mengine Duniani.
