Shirika la ndege tanzania atcl limezindua rasmi safari za ndege kutoka dar es ealam kwenda Afrika kusini Johansburg, ndege aina ya air bus 220 ndio itatumika zaidi katika safari hizi.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari hii ya kwanza kwenda afrika kusini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa amesema hatua hii ni muhimu wakati huu ambao serikali imejizatiti kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Uzinduzi wa safari hii ni ishara ya kuongeza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi lakini pia ni miongoni mwa vituo muhumu vitakavyoongeza idadi ya watalii nchini Tanzania.
Mkurugenzi ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi amesema safari hizi zitafanyika mara tatu kwa wiki yaani ijumaa,jumatatu na jumapili lakini bado shirika limejipanga kuanza safari za kwenda india katika mji wa mumbai mwezi ujao ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa na kuongeza kuwa huo ni mwazo wa safari nyingine za kuelekea nchini india kwenye mji wa Mumbai na China kwenye mji wa Gouanzu.