ATAKAEANDAMANA KILIMANJARO KUKAMATWA

0
172

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limesema halitosita kuchukua hatua kali dhidi ya kundi lolote ambalo litafanya maandamano kwa kushinikiza kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Hayo yamesemwa mjini Moshi na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kamanda Maigwa amesema kumejitokeza kikundi cha watu wachache wenye kusambaza taarifa mitandaoni zenye uchochezi na viashiria vya uvunjifu wa amani wenye kushinikiza kufanyika kwa maandamano hayo.

“Jeshi la polisi liko imara na halitasita kumchukulia hatua kali mtu yoyote ambaye atahatarisha usalama mkoani hapa,” ameonya Maigwa.

Amesema suala la Mbowe kukamatwa liko mahakamani hivyo waiachie mahakama ifanye kazi yake, kwamwe wananchi wasijihusishe kwa namna yoyote na watu wenye nia ovu na mkoa.