Askofu Malasusa ; Sensa ni agizo la Mungu

0
81

Viongozi dini pamoja na waumini wa dini mbalimbali nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la sensa ya Watu na Makazi litakayofanyika Agosti 23 mwaka huu.

Wito huo umetolewa mkoani Dar es Salaam na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa wakati wa kongamano la viongozi wa dini kuhusu sensa ya Watu na Makazi.

Amesema kiuhalisia kazi ya kuhesabu ni kazi ya Mungu hivyo viongozi wa dini wana wajibu wa kushiriki na kusimamia kila hatua kwa ukamilifu, maana ni jambo ambalo Mungu ameliruhusu.

Dkt. Malasusa ambaye pia ni mlezi wa Kamati ya Amani amesema dini zote zinaelekeza kuwa na takwimu ili kusaidia kuhudumia wafuasi wao, hivyo kama Watanzania wanapaswa kushirikk katika kuhesabiwa ili Taifa lipate takwimu sahihi zitakazowezesha katika kupanga mipango ya maendeleo

Ameelezea matumaini yake kuwa Watanzania wengi watajitokeza kuhesabiwa ikiwa ni kutii mamlala ambazo zimekuwa zikiwataka kufanya hivyo, huku wakizingatia kuwa hata vitabu vya dini vinasisitiza kutii mamlaka.