Askari watakiwa kutenda haki

0
151

Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Awadhi Haji, amewataka askari wa jeshi hilo kutenda haki kwa wananchi.

Kamishna Awadhi amesema hayo mkoani Arusha alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo, ambapo amewataka viongozi wa Jeshi la Polisi wa mkoa huo kusimamia vema maelekezo ya mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ambayo aliyatoa mara tu alipopewa dhamana ya kuliongoza jeshi hilo.