ASKARI POLISI & MAGEREZA WAONGEZEWE MUDA WA KUSTAAFU

0
165

Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Balozi Ernest Mangu amesema moja ya mapendekezo kutoka Tume ya Haki Jinai ni kuongeza muda wa kustaafu kwa Askari Polisi na Magereza ili nao wafanane na watumishi wengine

Balozi Mangu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kongamano la majadiliano ya Tume ya Haki Jinai lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkoani Dar es Salaam.

Amesema “eneo jingine tulilopata malalamiko ni malipo ya mafao ya mkupuo, yani haya yametolewa sana na Askari Polisi na pamoja Askari wa Magereza walikuwa wanalalamikia kile kikokotoo kina kula hela yao yote sasa wanaomba Serikali iondoe hicho kikokotoo, sasa sisi kwa sababu hatukuwa na uwezo wa kufanya hivyo tulitoa pendekezo.”

Ameeleza kuwa Askari Polisi na magereza wanalalamika zaidi kuliko watumishi wengine wa umma kwa sababu wenyewe huwa wanafanya kazi hawafiki miaka 60 katika utumishi wao wanaishi miaka 50 na 55, na huko nyuma ilikuwa miaka 40, 45 hadi 55 sasa ukimchukua huyo na yule aliyefika miaka 60 muda wakutumika unakuwa mfupi pesa yake ikija kuguswa na hicho kikokotoo inazidi kushuka chini zaidi.

“Kwa hiyo sisi moja ya pendekezo ni kwamba umri wa kustaafu kwa hawa askari polisi na magereza uwe miaka 60 kama watumishi wengine wa Umma,” amesema balozi huyo.