Asilimia 85 ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne wafaulu

0
178

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA ) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2020 yanayoonesha asilimia 85 ya Wanafunzi waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Matokeo hayo yametangazwa jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde, ambaye amesema kuwa Watahiniwa 434,654 walifanya mtihani huo na 373, 958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali.

Amesema kwa mwaka 2020, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 5.19.