Ashikiliwa kwa kukutwa na sare za JWTZ

0
115

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikiliia
Daniel Ruzinokwa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambazo amekuwa akizitumia kufanya udanganyifu na matukio ya uhalifu katika mikoa mbalimbali nchini.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema Ruzinokwa aliwahi kuwa askari wa JWTZ na baadaye kufukuzwa, lakini hakurudisha sare hizo.

Amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akizitumia sare hizo kufanya utapeli wa fedha kwa kuwalaghai watu, na kuwaahidi atawapeleka mafunzo ya usalama wa Taifa nchini Israel.

Kamanda Maigwa amesema Jeshi la Polisi limefanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kukuta akiwa na kombati za Jeshi, kofia za pama, kofia za chepeo, mikanda miwili ya Jeshi, koti la mvua na kitambulisho cha JWTZ, vyote vikiwa mali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.