Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Frank Mwaisumbe amesema kwa mara ya kwanza wilaya hiyo imepata kiwanda cha kuchakata mazao ya mifugo.
Amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuuza tani za nyama elfu kumi kwa siku ndani na nje ya nchi na kuwawezesha wafugaji kunufaika kwa kuongeza uchumi.
Mwaisumbe amesema kwa sasa jamii ya wafugaji itapata soko la uhakika kupitia kiwanda hicho, hata hivyo wanahitaji wawekezaji zaidi ambapo kiwanda kitakuwa na uwezo wakukusanya Bilioni 22 kwa mwaka.
