Arusha yaongoza matatizo ya Moyo

0
192

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge ameitaka jamii kuacha tabiabwete ambayo ndio chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo.

Akizungumza kwenye kambi ya matibabu jijini Arusha Kisenge ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti wa JKCI amesema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 17 kila mwaka hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Amesema wagonjwa wengi wa magonjwa ya Moyo wamekuwa wakitokea mkoa wa Arusha, hivyo kambi hiyo maalumu itasaidia katika ufumbuzi wa ukubwa wa tatizo hilo lakini pia itafanyika katika maeneo mengine ya nchi.

Mganga Mkuu Msaidizi Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center, Dkt. Wailece Adam amesema kliniki ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo na matibabu unaoratibiwa na JKCI, itaisaidia wakazi wa mkoa huo kutambua afya pamoja na kuokoa gharama za matibabu.