Arusha: Viongozi wa eneo palipokamatwa bangi wasimamishwa kazi

0
564

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amewasimamisha kazi mtendaji wa kata na mtendaji wa kijiji waliopo katika maeneo yaliyovunwa bangi wilayani Arumeru kupisha uchunguzi.

Mbali na wawili hao RC Kimanta ameagiza afisa tarafa awekwe chini ya uangalizi kutokana na kushindwa kuchukua hatua ya kufichua watu wanaojihusisha na kilimo cha bangi.

Kimanta amechukua hatua hiyo baada ya kukutana na maafisa tarafa na kata zilizopo katika wilaya hiyo, na amemtaka mkuu wa wilaya kupitia kamati ya ulinzi na usalama kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha na kilimo hicho.

Katika hatua nyingine amewataka wakuu wa idara za halmashauri kufanyakazi bila kubaguana.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema watendaji wa kata na vijiji wanatakiwa kuwafichua watu wanaojihusisha na kilimo cha bangi. Kwa upande wa watendaji hao wamesema watayafanyia kazi maelekezo waliyopokea.