ARIPO yasisitiza ulinzi wa bunifu

0
122

Waandishi wa habari na maafisa habari Barani Afrika, wameshauriwa kuandika na kutoa taarifa sahihi kuhusu Miliki Bunifu.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya mawasiliano kuhusu Miliki Bunifu yanayofanyika Harare, Zimbabwe, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miliki Bunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), Bemanya Twabaze amesema, Afrika ina wabunifu wengi lakini hawana ulinzi wa bunifu zao.

Amewataka waandishi wa habari kuendelea kutoa taarifa sahihi kuhusu umuhimu wa kulinda bunifu.

Mafunzo hayo ya mawasiliano kuhusu Miliki Bunifu yaliyoanza hii leo yanafanyika kwa muda wa siku tatu, ambapo zaidi ya waandishi wa habari 60 kutoka nchi 22 wanachama wa ARIPO wanashiriki katika mafunzo hayo.