Anwani za Makazi kusaidia zoezi la ukusanyaji kodi

0
176

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kwa kufanikisha zoezi la mfumo wa anwani za makazi

Rais Samia ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akihutubia katika kikao kazi cha wakuu wa mikoa kuhusu mfumo wa anwani na makazi kilichofanyika Jijini Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika kikao kazi cha wakuu wa mikoa Dodoma

Aidha Rais Samia amesisitiza elimu zaidi itolewe ili kuifanya Tanzania kufaidika na mifumo ya TEHAMA huku akisisitiza upanuzi wa mkongo wa Taifa kwa ajili ya matumizi ya mfumo huo katika halmashauri zote nchini

Rais Samia amesema mfumo huo wa anwani za makazi utasaidia katika zoezi la ukusanyaji kodi na kuongeza pato la Taifa

Rais Samia ametoa wito kwa Wizara zote zinazoguswa na mfumo huo ikiwemo TAMISEMI na Wizara ya Ardhi kuhakikisha zoezi hilo linakuwa na matokeo chanya kwa Taifa na kuwashirikisha wananchi

Kuhusu zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika mwezi wa 8 mwaka huu Rais Samia amesema kukamilika kwa mfumo huo wa anwani za makazi kutasaidia zoezi la hesabu ya watu na makazi kufanyika kwa urahisi na kuibadilisha Tanzania kuwa yakidijitali kwa kuwa na postikodi kwa ajili ya utambuzi wa kila mwananchi