Ambros akamatwa na meno ya tembo

0
172

Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia Reginald Ambros maarufu Amsi (42), kwa tuhuma za kukutwa na vipande viwili vya meno ya tembo alivyokua amevifunga ndani ya boksi.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema Ambros amekamatwa katika kijiji cha Endabashi wilayani Karatu.

Kamanda Masejo amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali.

Jeshi la polisi mkoani Arusha linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ili kupata mtandao mzima wa biashara hiyo.