Mwanamke mmoja huko Louisiana nchini Marekani aliyeganda na staili moja ya nywele kwa zaidi ya mwezi sasa baada ya kutumia gundi ya ujenzi apata msaada wa daktari bingwa.
Tessica Brown alijizolea umaarufu baada ya kurusha mtandaoni video akilalamika na kuonya watu kutokutumia gundi aina ya ‘Gorilla Super Adhesive’ na kusema si wazo zuri “bad idea.”
Brown anasema alitumia gundi hiyo baada ya kuishiwa na gundi maarufu ya nywele ya ‘Göt2B’ na kudhani Gorilla ingetoka akiiosha baada ya saa chache.
Mitandaoni video hiyo iliibua maneno ya kila aina huku wengine wakimcheka na wengine kumpa ushauri wa namna mbalimbali za kutoa gundi hiyo kichwani bila mafanikio.
Siku chache nyuma Brown alifanikiwa kukutana na daktari katika hospitali moja nchini humo aliyemsaidia bila mafanikio na baadaye aliamua kukata mkia wa nywele zake.
Aina ya gundi aliyotumia Tessica ni gundi isiyoingiza maji (waterproof) inayopakwa kwenye sakafu ya mbao, kugundisha tiles na kazi nyingine za kiufundi.
Brown amefanikia kuonana na daktari Michael Obeng wa hospitali ya Blev Hills aliyebobea kwenye upasuaji wa plastiki (Plastic surgeon) na kufanikiwa kuondoa gundi hiyo.