Aliyegeuza mti kuwa makazi Unguja kuchunguzwa

0
207

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein, amewaagiza wakuu wa mikoa visiwani humo kuwajibika ipasavyo katika suala la ulinzi na usalama, kwa kuhakikisha hakuna mgeni au mwekezaji anayefanya shughuli zinazoashiria uvunjifu wa amani na kuingilia usalama wa nchi.

Rais Shein ametoa agizo hilo mjini Unguja kufuatia taarifa ya kuwepo kwa raia wa kigeni aliyegeuza mti wa mbuyu kuwa sehemu yake ya makazi katika eneo la Pete, huku kukiwa na viashiria kadhaa vinavyohatarisha usalama wa nchi katika makazi hayo.

Ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini uhalali wa mgeni huyo kuwepo nchini na kumiliki eneo hilo pamoja na vifaa mbalimbali, vinginevyo hatua za kiusalama zichukuliwe dhidi yake.