Akiba ya fedha za kigeni inatosheleza miezi 4.4

0
118

Wizara ya Fedha na Mipango imesema hadi kufikia Aprili 2023 akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2023/2024.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hadi kufikia Aprili 2023, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa Dola za Kimarekani Bilioni 4.88 ambayo inatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takribani miezi 4.4.

Aidha, Waziri Nchemba amesema mahitaji ya nchi kisheria ni kuwa na kiasi cha fedha za kigeni kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa muda usiopungua miezi 4.